Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.6.2016 SAA 12:33 JIONI
Timu gani
itasonga mbele kwa kuingia hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam
(Azam Sports Sports Federation Cup) kati
ya Young Africans na Kiluvya United?
Majibu
ya swali hilo yatakatikana kesho Machi 7, 2017 baada ya mchezo kati ya timu
hizo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Utakuwa ni mchezo wa
kukamilisha raundi ya sita ambayo ilikutanisha timu 16 Bora na inayofanya vema
huingia hatua Nane Bora au Robo Fainali.
Mshindi
kati ya timu hizo, itaungana na timu nyingine saba zilizotangulia kucheza Robo
Fainali ambazo ni Simba na Azam FC za Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza,
Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha, Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda
FC ya Mtwara.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa
kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni. Bingwa wa michuano hiyo, ndiye
atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total
wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye
michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.
0 Comments