Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.6.2016 SAA 01:41 USIKU
Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi
wa Ligi Tanzania (Kamati ya Saa 72), katika kikao chake cha Machi 4, 2017
iliptia
matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017
inayoendelea hivi sasa.
Katika mechi namba 169 kati ya Simba
na Young Africans iliyochezwa Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, Young Africans iliingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.
Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha
kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa
kutumia milango rasmi.
Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14
(48) ya Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini
tano).
Katika kikao hicho kilifuta kadi ya
kwanza ya njano aliyoadhibiwa mchezaji Obrey Chirwa wa Young Africans wakati
timu hiyo ilipocheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka
huu.
Kadi hiyo imefutwa kwa mujibu wa
kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa kutolewa kwa Chirwa kwa
sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.
Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi
nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi ya
njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.
Kufutwa kwa kadi ya njano ya kwanza,
kunapelekea kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo ulisababisha
kadi nyekundu hivyo mchezaji angempaswa kukosa mchezo mmoja. Hata hivyo, kadi
ya pili ya njano inahesabiwa.
0 Comments