Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.MARCH.9.2016 SAA 11:19 JIONI
Mshambuliaji wa Yanga,Obrey Chirwa akioneshwa kadi ya pili ya njano na mwamuzi Ahmada Simba,picha na www.facebook.com/Sports.Eye |
Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na
Usimamizi wa Ligi za Tanzania (Kamati ya Saa 72), imemwondoa Mwamuzi wa kati,
Ahmada Simba
katika orodha wa waamuzi watakaochezesha mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.
Hatua hii imefikiwa baada ya utetezi
wa Mwamuzi Simba kudai kwamba hakuona tukio la Mchezaji wa Young African, Obrey
Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa na kumwonya
mchezaji kwa kadi njano.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo
ambao Young Africans walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa,
Machi mosi, mwaka huu.
Katika hiyo ya njano ilikuwa ni ya
kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta kadi hiyo kwa
mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa kutolewa kwa
Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.
Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi
nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi ya
njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.
Kufutwa kwa kadi ya njano ya kwanza,
kunapelekea kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo ulisababisha
kadi nyekundu hivyo mchezaji angempaswa kukosa mchezo mmoja. Hata hivyo, kadi
ya pili ya njano inahesabiwa.
Kadhalika uamuzi mwingine ulikuwa ni
kuipiga faini Young Africans iliyocheza na Simba Februari 25, 2017 kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Wanajwani hao kuingia uwanjani
kwa kutumia mlango usio rasmi.
Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha
kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa
kutumia milango rasmi. Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya Ligi Kuu,
Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini tano).
0 Comments