Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 9.2016 SAA 07:23 USIKU
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer) ya
Tanzania imeifunga Uganda mabao 7-5 katika mchezo
wa kirafiki wa
kimataifa uliofanyika leo Ijumaa Desemba 9, 2016 kwenye Viwanja vya
Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Jackson Msilombo, Kessy Ngao, Heri
Sassii na mtunza muda, Idd Maganga mabao ya Tanzania yalifungwa na
Samwel Opanga aliyefunga la kwanza, la sita na saba wakati mengine
yalifungwa na Kashiru Salum, Ally Babby na Ahmada Abdi aliyefunga
mawili.
Mabao ya Uganda yalifungwa na Emma Kalyowa aliyefunga bao la kwanza
na la tatu wakati mengine walifungwa na David Kassa, Naturinda Ambrosse
na Ochero Sulaimani.
Mchezo huo unaotambuliwa na CAF na FIFA, uliovutia mashabiki wengi
wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ulilenga kuziandaa timu hizo kujiandaa na michuano ijayo
ya kimataifa ndani ya bara la Afrika na ile la CAF.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Beach Soccer, John Mwansasu amesema huu ni
mwanzo mzuri wa kuiandaa timu yake na kufikia mafanikio ya juu katika
soka la ufukweni hivyo kuwaomba wadau kuzidi kuwaunga mkono.
Hivi karibuni kikosi hiki kilicheza na Ivory Coast katika michezo
miwili ya kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio.
0 Comments