Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 9.2016 SAA 07:23 USIKU
Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na
vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji
imebaini mambo
yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:
1. Mchezaji Hassan Hamis Ramadhan au Hassan Kessy alikuwa na Mkataba na Klabu ya Simba uliokuwa unaishia tarehe 15/06/2016.
2. Young Africans SC walikiri mbele ya Kamati kupeleka jina la
Mchezaji Hassan Ramadhani Kessy huko Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) tarehe 10/06/2016 huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na
klabu ya Simba.
3. TFF kupitia Sekretarieti yake ilikuwa na nafasi ya kuweza
kuielekeza Young Africans SC hatua stahiki za kuchukua ikiwa ni pamoja
na kuwasiliana na Klabu ya Simba kama taratibu zinavyoelekeza. Kama
hatua hii ingechukuliwa kwa wakati mwafaka mgogoro huu usingekuwa na
sura ya sasa na pengine usingekuwepo.
4. Simba SC walileta machapisho yanayotokana na Mtandao/blog wa mtu
waliomtaja kuwa ni Bin Zubeiry ukimwonyesha Mchezaji yuko na viongozi wa
Young Africans.
5. Young Africans SC ilionesha Mkataba iliosainiwa na Hassan Hamis
Kessy tarehe 20/6/2016 na hivyo hakukuwa na sababu ya msingi ya kufanya
mambo yaliyoainishwa kwenye kipengele cha 2 and cha 4 kabla ya
kumalizika kwa mkataba kati mchezaji Haasan Kessy na Klabu ya Simba.
6. Bila kuathiri hadhi ya Uanachama wengine wa TFF, Klabu ya Simba ni
brand kubwa kama ilivyo Klabu ya Young Africans, umakini mkubwa upaswa
kutumika katika kushughulikia brand hizi ili kuepuka madhara yasiyokuwa
ya lazima.
HATUA:
Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa
klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na
mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi
kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama
wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza
kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania.
Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni
tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000
(Shilingi milioni hamsini).
Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya
Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe
kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua
stahiki ziweze kuchukuliwa dcidi yake.
0 Comments