Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YAMPIGIA MAGOTI RAIS MAGUFULI,PIA YATANGAZA KAMATI MPYA YA MASHINDANO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.6,2016 SAA 12:47 JIONI

Mambo makubwa yaliyojili hii leo katika mkutano wa waandishi wa Habari wa klabu ya Simba ni pamoja na kutangaza kamati mpya ya
mashindano.ambayo tayari imeshaanza kazi rasmi.

Ofisa habari wa klabu iyo Haji Manara amesema wanaamini kamati hiyo itaweza kufanikisha shughuli zote za mashindano ambazo klabu itashiriki msimu huu.

Klabu ya Simba pia hii leo kupitia kwa Rais  wa klabu hiyo Evans Aveva ,kamati ya utendaji,sekretaliet,bechi la ufundi, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo,wamemuomba radhi rais magufuli kupitia kwa waziri nape, kwa kitendo kisicho cha kiuungwana cha mashabiki wake kuvunja viti uwanjani .

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alitangaza kuvipiga marufuku klabu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana.

Waziri Nape alitangaza kuchukuwa uamuzi huo baada ya kutembelea uwanja wa Taifa na kubaini uharibifu mkubwa unaosemekana kufanywa na  mashabiki wa Simba waliong'oa Viti katika  uwanja wa Taifa wakati wa mechi ya watani hao wa  jadi mchezo uliopigwa October 1 na kumalizika kwa sare ya 1-1.  

Takribani Viti 1,781 vilivyokuwa katika jukwaa la klabu ya Simba Vimeng'olewa siku ya jana katika mchezo huo
 

Simba wamemuandikia barua rais magufuli ya kuomba radhi,

Simba wamesema endapo watabaini kama waliofanya uhalifu huo ni wanachama wao basi watachukuwa hatua za kinidhabu kwa wanachama hao,huku klabu hiyo ikiaamini rais atawaruhusu kutumia tena uwanja wa taifa  kwa kuwa ni waelewa.

Katika Hatua nyingine Klabu ya Simba pia kupitia kwa msemaji wao Haji Manara wametoa ombi kwa bodi ya ligi na Tff kuhakikisha wanachagua waamuzi sahihi wa kuchezesha mechi kubwa.

Simba wamesema wapo  tayari kugharamia malipo ya waamuzi kutoka nje ya Nchi kuchezesha mechi zao kama ikibidi swala hilo.


KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments