Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Lady Jaydee (Comando) siku ya Jumapili Jun 26 alikuwa ni mmoja wa watu waliojitokeza
kuipa sapoti Timu ya taifa ya vijana ya Tanzaia chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys Katika uwanja wa taifa.Lady Jaydee akiwa pamoja na meneja wake Seven Mosha |
Lady Jaydee ambaye yuko katika chat na nyimbo yake ya Ndi ndi ndi alishuhudia mchezo huo akiwa pamoja na meneja wake Seven Mosha waliishuhudia Serengeti Boys ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa raundi ya Kwanza kufuzu Fainali za U17 Afrika mwakani Madagascar.
Mchezaji wa Serengeti Boys akimtoka beki wa shelisheli |
Serengeti boys wakishangilia bao la kwanza |
ANGALIA PICHA
Katika
mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
salaam,Serengeti Boys walitawala asilimia kubwa ya mchezo, na Mabao yao
mawili yalipatikana katika kipindi cha kwanza,bao la
kwanza likipatikana katika dakika ya 15 likifungwa na Dickson Nickson Job.
Bao la pili la Serengeti Boys alifunga
Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 21 baada ya kuingiza mpira nyavuni
uliotemwa na kipa Gino Pleursuse wa Seychelles (Shelisheli) ambaye
alipigiwa shuti kali na Ally Hamis Ng'anzi.
Kipindi cha pili kilianza kwa Serengeti Boys kuonekana bado wakiutawala mchezo huo na
katika dakika ya 14 mchezaji wa Seychelles (Shelisheli) aliunawa mpira
katika eneo la Hatari na Refa kutoka Ethiopia Belay Tadesse Asserese
kuamua penati ipigwe,na Ally Hussen Msengi akaweka nyavuni Penati hiyo
dakika ya 15 na kuipatia Serengeti Boysbao la Tatu.
0 Comments