Baadhi ya mashabiki waliojitambulisha kama wanachama wa
klabu ya Simba, wamejitokeza kwenye mkutano wa waandishi wa habari
katika makao
makuu ya klabu ya Young Africans na kuwataka Wanasimba kujitokeza kwa wingi na
kuwaunga mkono mahasimu wao iunga mkono Yanga, kesho.
Yanga inashuka dimbani kuivaa TP Mazembe katika mechi ya
Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Kutoka kushoto:Amaniel Mngonja na Rifat Maulanga wamejitokeza kwenye mkutano huo ulioongozwa na Msemaji wa Yanga, Jerry Muro |
Amaniel Mngonja na Rifat Maulanga wamejitokeza kwenye
mkutano huo ulioongozwa na Msemaji wa Yanga, Jerry Muro katika makao makuu ya
Yanga, Kaunda na Twiga jijini Dar es Salaam.
Rifat Maulanga amesema wameona kuna haja ya kuweka itikadi
zao pembeni na kuangalia uzalendo wa taifa la Tanzania ambalo kwa sasa
linawakilishwa na Young Africans katika medani ya kimataifa.
Kutoka kushoto:Amaniel Mngonja na Rifat Maulanga na Msemaji wa Yanga, Jerry Muro wakiimba nyimbo kuonesha uzalendo |
Naye Amaniel Mngonja amesema anaamini kwa kesho kuna
umuhimu wa jambo la utaifa likatangulizwa mbele, hivyo amewataka wanasimba
wenzake popote pale walipo kuwaunga mkono Young Africans.
SIKILIZA HAPA
Baada ya taarifa za mashabiki wa soka kuruhusiwa kuingia
bure katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, katika mchezo wa kesho wa
kombe la shirikisho kuonekana katika mitandao ya kijamii, uongozi wa klabu ya
Young Africans umethibitisha ukweli wa jambo hilo katika mkutano na waandishi
wa habari.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Young Africans,
Jerry Muro amesema maamuzi ya kutoweka kiingilio katika mchezo wa kesho
yamechukuliwa na uongozi wa klabu hiyo kutokana na kuona umuhimu na kutambua
mchango wa mashabiki wa soka nchini ambao wamekua wakiwaunga mkono katika
jitihada za kuleta maendeleo.
Hata hivyo Jerry Muro ametoa wito kwa mashabiki
watakaokwenda uwanjani hiyo kesho kuhakikisha wanavalia mavazi yenye rangi za
njano na kijani ama yenye rangi za bendera ya taifa, ili kuonyesha uzalendo kwa
vitendo.
0 Comments