Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.6,2016 SAA 01:09 USIKU
Hii leo Klabu ya soka ya azam leo
imemtambulisha Abdul Mohamed Kuwa
maneja mkuu wa timu hiyo.
Akizungumza katika utambulisho huo mtendaji mkuu wa waoka
mikate hao Saad Kawemba amesema wameamua kumuongeza abdul kutokana na kuongeza
ufanisi wa utendaji wa timu hiyo hasa ukizingatia klabu hiyo ina malengo ya
kimataifa Zaidi.
Kawemba amemtangaza Abdul ambaye alikuwa mwana habari kutoka
shirika la utangaji la BBC huku akisema kuwa Abdul ni miongoni mwa
wanafamilia wa azam fc.
Kwa upande wa maneja mpya wa klabu hiyo Abdul Mohamed
amesema ameingia kwenye klabu hiyo kuiongoza timu hiyo kwa lengo la kuito Azam
Fc hapo iliopo na kuipandisha juu klabu hiyo.
Majukumu ya kuendesha klabu kila siku yamekuwa na changamoto mpya zinazohitaji kutatuliwa kupitia nguvu kazi ya watu na Azam FC imesema haitasita kuboresha mfumo wake wa uendeshaji wa klabu ili kuendana na changamoto hizo, kwa kuuongezea nguvu kazi pale inapohitajika ili kufikia mafanikio.
Mbali na kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye sekta ya habari akipita IPP Media, Clouds Media na BBC, Mohamed pia amesomea masuala ya Uhasibu na Fedha. Azam FC inamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya hayo katika ngazi ya soka.

0 Comments