Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.18,2016 SAA 11:33 JIONI
Wakati leo Jumanne Oktoba 18, 2016 timu ya JKT Ruvu ya Pwani na
Kagera Sugar zinafungua rasmi mzunguko wa 11 wa Ligi Kuu ya
Mpira wa
Miguu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), michezo mingine sita itafanyika
kesho Jumatano Oktoba 19, mwaka huu wakati keshokutwa Alhamisi Oktoba
20, kutakuwa na mchezo mmoja tu.
Mchezo wa leo Na. 86 wa VPL utafanyika Uwanja wa Mabatini mkoani
Pwani kabla ya kesho Oktoba 19, mwaka huu kuendelea kwa mechi sita pia
za mzunguko 11 wa kukamilisha raundi ya kwanza kwa msimu 2016/17.
Vodacom – Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza nchini kwa kutoa
huduma za kisasa za mawasiliano ndiyo mdhamini mkuu ligi hiyo
ikisaidiana kwa karibu sana Kampuni ya kisasa ya vyombo vya habari yenye
kurusha vipindi vyake kwa weledi na ubora wa hali ya juu ya Azam
Televisheni (Azam Tv) na DTB- Benki ya kuaminika nchini kwa usalama wa
fedha zako.
Kampuni hizo zinazong’arisha VPL, kesho zitakuwa sambamba kwenye
kuchagiza michezo ya Ruvu Shooting ya Pwani ambayo itaikaribisha Mwadui
ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Mabatini uliuoko Mlandizi mkoani Pwani
katika mchezo Na. 81 wa VPL utakaoanza saa 10.00 jioni.
Mchezo Na. 82 utakaozikutanisha Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa
Sugar ya Morogoro utafanyika saa 1.00 usiku (19h00). Mchezo huo
utafanyika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi – maskani ya Azam yalioko nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati mchezo Na. 83 utazikutanisha timu
za Ndanda FC na Mbeya City ya Mbeya kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona
mjini Mtwara.
Mchezo Na. 85 utazikutanisha timu za Tanzania Prisons ya Mbeya na
Stand United itakayokuwa mgeni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
jijini Mbeya huku mechi Na. 87 itazikutanisha Toto African ya Mwanza
itakayocheza na Young Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza wakati African Lyon itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye
Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kwenye mchezo Na. 88.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kutwa Alhamisi Oktoba 20, kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambako vinara wa ligi hiyo kwenye msimamo
hadi sasa, Simba itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza katika mchezo
Na. 84.

0 Comments