Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.18,2016 SAA 10:25 JIONI
Mshambuliaji Shiza Kichuya wa Simba SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa Septemba msimu wa
2016/2017.
Kichuya ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.
Mchezaji aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12
katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee
kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. Pia alifunga mabao matatu
katika mechi mbili kati ya nne ilizocheza timu yake.
Kwa kushinda tuzo hizo ya mwezi, Kichuya
atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini
wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

0 Comments