Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.18,2016 SAA 11:58 JIONI
Timu 24, zinatarajiwa kupambana katika michuano ya Ligi Daraja la
Pili msimu wa 2016/17 kuanzia Oktoba 29, mwaka huu,
imefahamika.
Timu hizo zimepangwa katika makundi manne yenye timu sita kwa
kuangalia zaidi jiografia au kanda ambako timu imetoka – lengo likiwa
kupunguza gharama kwa timu shiriki hasa ikizingatiwa kuwa michuano hiyo
haijapata mdhamini hadi sasa.
Kundi A lina timu za Mashujaa ya Kigoma, Mirambo ya Tabora, Mji Mkuu
ya Dodoma, Green Warriors ya Pwani, Bulyanhulu na Transit Camp za
Shinyanga.
Mechi za kwanza zitakuwa ni kati ya Mashujaa dhidi ya Green kwenye
Uwanja wa Tanganyika mjini Kigoma wakati Mirambo itaikaribisha Mji Mkuu
kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Timu za Transit Camp na Bulyanhulu
zitacheza Oktoba 30, mwaka huu.
Kundi B; African Wanderers ya Iringa itaikaribisha AFC ya Arusha
kwenye Uwanja wa Kichangani mjini Iringa siku ya Oktoba 29, 2016 wakati
Kitayosa itakuwa mgeni wa Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
jijini Arusha. Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Pepsi ambayo itacheza
na JKT Oljoro Oktoba 30, mwaka huu.
Kundi C; Villa Squad itafungua dimba na Kariakoo ya Lindi kwenye
Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam wakati Burkinafaso ya
itaikaribisha Abajalo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Timu
nyingine kwenye kundi hilo ni Cchanganyikeni na Cosmopolitan za Dar es
Salaam.
Kundi D; Namungo ya Lindi itafungua dimba na Sabasaba kwenye Uwanja
wa Sokoine ulioko Nachingwea mkoani Lindi wakati Mkamba Rangers itakuwa
nyumbani kwenye Uwanja wa Mkamba kuikaribisha Mawenzi Market kwenye
Uwanja wa Mkamba ulioko Morogoro.

0 Comments