Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.19,2016 SAA 11:45 JIONI
![]() |
| Juma Amir Maftah kulia enzi zake akiitwa Pele wa Mwanza na Khalfan Ngassa.(PICHA NA shaffihdauda.co.tz) |
Idara
ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limethibitisha kuwa Kocha Khalfan Ngassa hana leseni yoyote kati
ya
Leseni ya chini kuanzia Daraja B ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani
Afrika (CAF) au Daraja C kwa Kocha Msaidizi pia kutoka CAF, hivyo hastahili kukaa kwenye benchi la timu ya Toto Africans
kama kocha mkuu au kocha msaidizi.
Afisa
habari wa shirikisho la soka nchini Tanzania Afred Lucas Ameiambia Jamii na Michzezo kuwa
Shirikisho hilo limewaandikia barua klabu ya Toto Afrika ya
kutomtumia kocha Khalfan Ngassa.
Kocha
Khalfan Ngassa amekuwa kwenye benchi la timu ya mpira wa miguu ya Toto
Africans ya Mwanza akiwa kocha msaidizi kwa mechi tatu mfululizo za Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inayoendelea kwenye viwanja
mbalimbali nchini.
Khalfan
Ngassa aliongoza timu kwenye mchezo Na. 62 dhidi ya Kagera Sugar Oktoba
7, 2016; mchezo Na. 67 dhidi ya Mbao FC uliofanyika Oktoba 12, 2016 na
Mchezo Na. 79 dhidi ya Majimaji ya Songea uliofanyika Oktoba 15, mwaka
huu.
Kitendo
kinachofanywa na Toto Africans ni ukikwaji wa kanuni na ni vema uongozi
wa Toto ukamwondoa Khalfan Ngassa kwenye benchi ili kuepuka adhabu.
Kipendele cha (7) cha kanuni hiyo ya 72, inaelekeza adhabu kuwa inaweza
kutozwa si chini ya Sh 500,000 (shilingi laki tano).
Pia
tunazikumbusha klabu zote kuwa kuanzia msimu ujao wa 2017/18 wa Ligi
Kuu ya Vodacom, kocha anayestahili kukaa kwenye benchi ni yule mwenye
leseni Daraja A kwa nafasi ya Kocha Mkuu na angalau Leseni Daraja B kwa
kocha msaidizi.

0 Comments