Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.12,2016 SAA 02:00 USIKU
ANGALIA PICHA
Ushindi huo umerejesha matumaini kwa mabingwa watetezi hao wa Ligi kuu Tanzania Bara
.
.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na winga Mzambia, Obrey Chirwa dakika chache kabla ya kwenda mapumziko.
Yanga walifanikiwa kupata bao la pili dakika ya 68 kupitia kwa Msuva kabla ya mshambuliaji aliyetokea benchi Donald Ngoma kufunga la tatu dakika ya 80 akimalizia pasi nzuri ya Mwashiuya.
Yanga ililazimika kumalizia pungufu baada ya mshambuliaji Amissi Tambwe kutolewa nje baada ya kugongana na Shaaban Nditi na kupasuka kwenye dakika ya 87.
Yanga sasa imefikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi saba, inazidiwa pointi sita na mahasimu wao wa jadi, Simba SC walio kileleni ingawa wamecheza mechi moja zaidi.
ANGALIA PICHA















0 Comments