Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta hii leo usiku ameisaidia timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji kujiweka
katika mazingira mazuri katika michuano ya kuwania kucheza Europa League kwa timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Buducnost Podgorica ya Montenegro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya mchujo mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.

Timu hizo zitarudiana Julai 21, mwaka huu Uwanja wa Pod Goricom mjini Podgorica nchini Montenegro na mshindi wa jumla atasonga mbele.
Samatta alifunga bao la pili katika dakika ya 79 huku bao la kwanza la Genk likifungwa kwa penalti na Neeskens Kebano dakika ya 17 ya mchezo huo.
0 Comments