Sakata la kufungiwa kwa Jerry Muro na shirikisho la soka nchini TFF, limezungumzwa na afisa habari wa klabu ya Simba, Haji
Sundey Manara kwa kusema mkuu huyo wa idara ya habari na mawasilino wa mahasimu wao katika soka la bongo aliponzwa na kuzungumza na kuvuka mipaka ya kazi yake.
Sundey Manara kwa kusema mkuu huyo wa idara ya habari na mawasilino wa mahasimu wao katika soka la bongo aliponzwa na kuzungumza na kuvuka mipaka ya kazi yake.
Manara amegusia suala hilo alipokutana na Jerry Muro alipomtembelea nyumbani kwake jana usiku sambamba na baadhi ya mashabiki na wanachama wa young Africans kwa lengo la kumkabidhi fedha za mchango kiasi cha Shilingi milioni moja na elfu hamsini na tano (1,055,000) kama mchango wao ambazo utasaidia kwenye matibabu yake atakapokwenda nchini India mwishoni mwa juma hili.
Mbali na kuzungumza udhaifu wa Muro ambao umemsababishia kufungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja, Manara pia alitoa shukurani kwa msaada wa fedha walioupokea kutoka kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa Young Africans.
SIKILIZA HAPA
Katika hatua nyingine Manara akafikisha ujumbe kwa wanachama na mashabiki wa Young Africans pamoja na Simba kuelekea katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili, ambapo mabingwa wa Tanzania bara watapambana na Medeama katika michuano ya kombe la shirikisho.
Naye Jerry Muro alizungumza kwa niaba ya wanachama na mashabiki wa Young Africans waliojichangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya Haji Manara, huku akisisitiza umoja na upendo miongoni mwa pande hizo mbili zinazo hasimiana katika medani ya soka hapa nchini.
0 Comments