Jose Mourinho amedai Romelu Lukaku ameondoka Chelsea kwa sababu mchezaji huyo alitaka kuwa na uhakika wa mara
kwa mara wa kuanza katika kikosi.
'
Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amesaini mkataba wa miaka mitano na Everton kwa uhamisho wenye gharama ya £ 28m na klabu hiyo aliyoitumia msimu uliopita kwa mkopo
na kufanya kuwa uhamisho uliovunja Rekodi kwa klabu hiyo.
na kufanya kuwa uhamisho uliovunja Rekodi kwa klabu hiyo.
Mourinho ilisema,"nafikiria mbali juu ya uamisho huu na ukweli ni kwamba Romelu mara zote yoko vizuri sana na sisi, katika mawazo yake, katika mbinu zake hakunishawishi sana kuja. na hali ya ushindani katika klabu ya Chelsea," alisema Mourinho.
"Alitaka kucheza Chelsea lakini ni wazi alitaka kuwa chaguo la kwanza kwa washambuliaji,ambapo katika klabu yenye mwelekeo wetu, ni vigumu sana kumuahidi mchezaji""Hivyo tukaacha mara moja nia yake ya kurudi kwetu"
Mourinho pia alisisitiza kuwa hana kinyongo chochote dhidi ya Lukaku na anamtakia kila la kheri kwa uhamisho wake huo wa kudumu kwa klabu hiyo ya Goodison Park kwa ada ambayo ni rekodi ya klabu hiyo inayonolewa na Roberto Martinez.
"Jambo muhimu ni yeye kuwa na furaha na mambo anayoyafanya. ni mtoto mzuri, "aliongeza Mourinho.
"Jambo moja tu ambacho tunaweza kufanya ni kumtakia mema"
Siku ya Jumatano Lukaku alindika ujumbe katika mtandao wa kijamii wa Twitter baada ya kuweka picha yake akiwa ameketi juu siti ya ndege, akionesha kidole gumba na tabasamu pana, pamoja na maelezo yaliyosomeka:. Muda wa kuanza ukurasa mpya"
0 Comments