Ticker

6/recent/ticker-posts

AFRIKA:BAADA YA HERVE RENARD KUTANGAZWA KUWA KOCHA MPYA WA IVORY COAST,FAHAMU MAJUKUMU YAKE,PAMOJA NA MKATABA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.JUL.05,2014 SAA 05:50 USIKU
Mfaransa Herve Renard ndiye kocha mpya wa  timu ya taifa ya Ivory Coast baada ya kudhibitishwa siku
ya Alhamisi, Herve Renard amechukuwa nafasi ya Sabri Lamouchi, ambaye alifukuzwa baada ya timu hiyo kushindwa kuendelea katika hatua ya makundi katika Kombe la Dunia  2014 nchini Brazil. 

Beki huyo wa zamani, ambaye aliongoza Zambia katika ushindi dhidi ya Ivory Coast katika Kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon 2012 , amepewa kazi ya kufanikisha kufuzu kwa Tembo hao  katika michuano ya  AFCON  2015 huko Morocco. 
Renard amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo anaweza kuongezewa mkataba mpya kulingana na utendaji wake wa kazi, kwa mujibu wa rais wa  FA ya Ivory Coast Augustin Sidy Diallo.

Rais wa chama cha soka nchini Ivory Coast alisema Renard ndiye mwenye mpango mzuri kwa nchi hiyo, na hata mshahara wake aliotaja unalipika, hivyo ndiye aliyestahili.
Rienard, 45, alichaguliwa miongoni mwa mwajina matatu ya mwisho, yaliyowajumuisha,kocha wa  zamani wa Benfica Jose Manuel De Jesus  kutoka Ureno na Frederic Antonetti, ambaye ni kocha wa zamani wa timu kutoka  Ufaransa, Rennes.

ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments