Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amevunja ukimya,baada ya kusema kwamba Fernando Torres hauzwa wakati wa
dirisha hili la uhamisho.
Mourinho ana washambuliaji watatu msimu huu baada ya kuwasili hivi karibuni kwa Diego Costa na kurudi kwa Didier Drogba lakini bosi huyo wa Chelsea anasisitiza wote hao watatu ni muhimu katika kikosi chake.
Torres anapigania nafasi yake ambayo ilimfanya asajiliwe na Chelsea kwa gharama ya £ 50m mwaka 2011 lakini katika mahojiano maalum na Sky Sports News Mreno huyo alisema: "Sisi tuna kikosi nzuri"
"Kikosi kamili kitakuwa na wachezaji 18, si 17 au 16, lakini sheria ni sheria na sisi tuna kazi ngumu, hata hapa, kwa kuwa hatutaki kuwa na aina ya matatizo katika siku zijazo".
"Tunataka kuwa na wachezaji wa English zaidi katika kikosi chetu ambao tutakuwa nao katika siku zijazo lakini katika wakati huu sisi bado tuko katikati mchakato huu".
"Hivyo ni wakati ambao tutafanya uamuzi kuhusu mchezaji mmoja kuondoka katika orodha hiyo."
Na alipoulizwa kama mchezaji huyu alikuwa Torres, kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 haraka alithibitisha kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania atasalia katika uwanja wa Stamford Bridge:
"Hapana washambuliaji watatu ni wa msingi katika kikosi na sisi tuna washambuliaji watatu; Fernando, Didier na Diego hivyo mmoja wao haiwezekani kuondoka kwa uhakika," aliongeza.
Na kuhusiana na msimu ujao, Mourinho alikataa kutaja makamu nahodha akidai mchezaji yeyote wa timu yake anaweza kuchukuwa jukumu hilo la nahodha wa muda mrefu John Terry.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments