Katika kikao chake cha 13 Julai 2016, Kamati ya
Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetoa msimamo
kuhusu suala la Stand United kama ifuatavyo:--
Kamati imepitia vielelezo vyote na kujadiliana na
wadau wa Stand United na kubaini bayana kwamba Stand United Football
Club, ndiyo jina sahihi na halali lililosajiliwa kwa Msajili wa Klabu na
Vyama vya Michezo.
-
Uchaguzi uliofanyika
hivi karibuni kwenye Klabu ya Stand United una sifa zote za kuitwa
uchaguzi huru na wa haki kwa vile mchakato ulihusisha wanachama halali
klabu hiyo.
-
Wanachama wa Stand United ambao hawakushiriki
uchaguzi ikiwa ni pamoja na wale waliokwenda kundi la kampuni wana
uhalali wa kuendelea kuwa wanachama wa Stand United.
-
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Stand
United FC ni halali na ni ruksa kwao kuendesha ofisi na shughuli za
Stand United kwa ujumla.
- Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania linatambua daftari la Wanachama wa Stand United lililoboreshwa kwa maelekezo ya TFF.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments