Ticker

6/recent/ticker-posts

MOURINHO ASEMA LIVERPOOL LAZIMA WAANGALIWE KWA UMAKINI,LAKINI AMUOMBEA MABAYA SUAREZ

 Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 29.2013 SAA 07:30 USIKU

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho anaamini kwamba Liverpool kutokuwepo na ushindani na Ulaya msimu huu  na ana maana kwamba
lazima kuzingatiwa ushindani wa kweli katika ligi kuu.
 
Liverpool walimaliza nafasi ya saba msimu uliopita, lakini wao wako imara katika msimamo wakitofautiana alama moja na Chelsea na  wanafunga safari hadi  Stamford Bridge siku ya Jumapili kupambana na vijana wa Jose Mourinho . 
Muhimu kwa wachezaji wao wa kuvutia wamekuwa wakifunga kama Luis Suarez, ambaye amepata kucheka na wavu mara 19 katika mechi 13 tangu arudi baada ya kupigwa marufuku kwa kumuuma mlinzi wa  Chelsea  Branislav Ivanovic wakati wa mchezo wao mwezi Aprili. 
Hata hivyo, wakati Mourinho ana ufahamu umuhimu wa Suarez kwa upande wa Brendan Rodgers, anasema kwamba uwezo wao hawawezi kuanza na kumaliza na mshambuliaji huyo wa Uruguay. 
Na hata hivyo Jose Mourinho aliendeleza ucheshi siku ya Ijumaa pale alipoashiria kwamba mshambuliaji matata wa Liverpool, Luis Suarez, huenda akakosa mechi dhidi yao Stamford Bridge Jumapili kutokana na ‘jeraha kiasi’  
Akiongea na runinga ya Chelsea, meneja huyo alidinda kutaja tukio tata la Suarez kwenye mechi yao ya mwisho Aprili pale Anfield ambapo straika huyo alipotia meno yake mkononi mwa mlinda ngome, Branislav Ivanovic. 

Badayake, Mourinho alielezea matumaini kuwa mshambuliaji huyo wa Uruguay- ambaye alipigwa marufuku ya mechi kumi kufuatia kisa hicho- atakosa mechi baina ya vilabu hivyo vinavyo miliki nafasi za tatu na nne kwenye Ligi ya Premier ya Uingereza.

“Pengine Suarez ana jeraha dogo,” Mourinho alisema akigusia kushindwa kwa Liverpool 2-1 safarini na Man City siku ya Alhamisi. “Siombi ajeruhiwe sana..jeraha dogo tu la kumfanya asicheze siku nne.” 

Mourinho, ambaye amehuzunishwa na ukame wa mabao kutoka wachambuliaji wake, alikataa kulinganisha uwezo baina yao.

Fernando Torres, Samuel Eto’o na Demba Ba, ambao ni mastraika wake wakuu, wamefunga mabao matano pekee kati yao. 

“Kila mechi ni ngumu,” alisema. “Tofauti ni kwamba timu zingine ni kubwa, jina kubwa, uwezo mkubwa… Man City- Liverpool, Chelsea-Liverpool, Chelsea-Arsenal…

“Kwenye mechi mbili za mwisho tulizocheza nyumbani, Swansea na Crystal Palace (tulishinda) 1-0, 2-1. Ni lazima utie bidii zote kushinda mechi.”

Mourinho alimsifu Eto’o licha ya kukosa nafasi mbili za wazi kufunga bao lake la tatu msimu huu. 

“Alifanya vyema. Nataka washambuliaji wangu wajihisi wanabuni nafasi na wafanyie hilo kazi. Nataka watume makombora, nataka golikipa aokoe au wagonge ulingo wa lango.”

 

Post a Comment

0 Comments