Uongozi wa klabu ya Young Africans umesema umeridhishwa na kiwango cha soka kilichoonyeshwa katika mchezo wao wa pili wa
michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika CAF dhidi ya TP Mazembe uliochezwa jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika CAF dhidi ya TP Mazembe uliochezwa jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino jerry Muro wamewasilisha taarifa za uongozi wa klabu hiyo kuridhishwa na uwezo wa kikosi chao kwa kusema kilicheza vyema wakati wote licha ya kukubali kufungwa katika kipindi cha pili.
Muro amesema kutokana na hali hiyo wamepokea taarifa kutoka CAF inayoonyesha tathmini ya mchezo huo na wamebaini kuna hatua kubwa waliyoipiga katika viwango vya ubora wa soka barani Afrika upande wa vilabu.
Muro pia amezungumzia maandalizi ya kikosi chao ambacho kitakab iliwa na mchezo wa tatu wa kundi A wa michuano ya kombe la shiriksiho, kati kati ya mwezi ujao kwa kupambana na Medeama Sporting Club kutoka nchini Ghana katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Kuhusu malipo ambayo yanapaswa kulipwa kwa ajili ya matumizi ya uwanja wa taifa ambao ulitumika kwa mchezo wa jana, Jerry Muro amekanusha taarifa zilizoibuliwa hii leo katika mitandao ya kijamii kwa kudai uongozi wa klabu ya Young Africans umetakiwa kulipa shilingi milion 530.
Amesema taarifa hizo sio rasmi, na mpaka mchana wa leo walikua bado hawajapokea barua yoyote kutoka wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo ambayo inawaagiza kulipa kiasi hicho cha pesa.
SIKILIZA HAPA
Wakati uongozi wa Young Africans ukitangaza msimamo huo wa kulipwa asilimi 15 pekee na si gharama nyingine zozote, shirikisho la soka nchini TFF limetangaza masikitiko yake, kufutia uharibifu uliofanywa na baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam hapo jana.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema uchunguzi wa awali ulioanza kufanywa mara baada ya mchezo huo kumalizika jana jioni umebaini kuwepo kwa uharibifu katika baadhi ya maeneo.
0 Comments