Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA JUU YA MWANARIADHA OSCER PISTORIUS

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Des.08,2015 SAA 11:43 JIONI
Mahakama
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ameachiwa kwa dhamana ya Rand 10,000, ambazo ni
takribani dola 700 hii leo, baada ya makahama kuu ya nchi hiyo Alhamis iliyopita, kumkutana hatia ya kumuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Barry Roux, wakili wa mwanariadha huyo anayekimbia kwa miguu ya bandia amesema wakati wa kuomba mteja wake kuachiwa kwa dhamana, kwamba watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo katika mahakama ya juu kabisa nchini Afrika Kusini. 

Pistorius anakabiliwa na kifungo cha muda usiopungua miaka 15 jela, baada ya mahakama kuu ya nchi yake kuibadilisha hatia ya kuuwa bila kukusudia na kuifanya mauaji ya makusudi. Kesi yake itasikilizwa tena tarehe 16 Aprili mwaka 2016.


Jaji Aubrey Ledwaba amesema hakuna hatari kwamba Pistorius anaweza kutoroka akipewa dhamana kwani alijiwasilisha mahakamani mwenyewe leo.

Ataendelea kutumikia kifungo cha nyumbani na atakuwa na kifaa cha kumfuatilia kielektroniki. Anaruhusiwa kuondoka nyumbani kati ya saa moja asubuhi hadi saa sita mchana katika eneo la nusu kipenyo la kilomita 20 kutoka kwa nyumba anamoishi.
Pistorius pia ametakiwa kusalimisha pasipoti yake kwa mahakama.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments