Mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia Ya Kongo pamoja na timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS, Mbwana
Samatta hii leo alifika ofisini kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kusaka Baraka za serikali ya awamu ya tano kabla hajaondoka nchini kuelekea nchini Nigeria katika hafla ya utoaji wa tuzo za Afrika.
Samatta hii leo alifika ofisini kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa ajili ya kusaka Baraka za serikali ya awamu ya tano kabla hajaondoka nchini kuelekea nchini Nigeria katika hafla ya utoaji wa tuzo za Afrika.
Mbwana Samatta akisaini kitabu cha wageni katika ofisini kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo |
Samatta amesema anaamini kusaka Baraka katika ofisi ya Waziri ambayo inawakilisha serikali ni utamaduni mzuri ambao aliukuta duniani na anaamini kwa kufanya hivyo ni hatua kubwa ya kufikia mafanikio anayoyatarajia.
Amesema lengo lake ni kuona anafanya vyema zaidi katika ukanda wa Afrika upande wa tuzo, pamoja na nje ya bara hilo ambalo siku sio nyingi atakwenda kucheza soka nchini Ubelgiji.
MSIKILIZE SAMATTA NA NAPE NNAUYE
Samatta pia akazungumzia mchakato wa uhamisho wake kutoka TP Mazembe kuelekea nchini Ubeljigi ambapo tayari baadhi ya taratibu zimeshakamilishwa ili aweze kujiunga na klabu ya FC Genk.
Kwa upande wake waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amempongeza Mbwana Samatta kwa hatua kubwa aliyofikia ya kuingia katika tuzo za wanasoka bora wa Afrika na amemuhakikishia serikali ya awamu ya tano kuwa nyuma yake katika jambo hilo.
Wakati huo huo Nape Nnauye akaendelea kuwapasha habari viongozi na wajanja wachache waliojipachika katika tasnia ya michezo kwa kutafuna jasho la wachezaji kwa maslahi yao binafsi kushtuka mapema ili waweze kujiondoa kabla hajawaumbua hadharani.
Mchambuzi wa habari za michezo Shafii Dauda akiwa na Mbwana Samatta |
Tuzo za wachezaji bora Afrika zitatolewa nchini Nigeria January 7, 2016 ambapo Samatta anawania tuzo hiyo ya mcheaji bora Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika akiwa pamoja na Bahgdad Bounejah (Etoile du Sahel, Tunisia) Algeria na Robert Kidiaba (TP Mazembe, Congo DR) Jina la Samatta limeingia kwenye orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake ya TP Mazembe kutwaa kombe la klabu bingwa Afrika huku yeye akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments