Klabu ya Simba tarehe 29 Desemba 2015 wamezungumza na waandishi wa Habari juu ya maswala Kadhaa kuhusiana na klabu
hiyo.
hiyo.
Mkuu wa kitengo cha habari wa Klabu hiyo Haji Manara ameongelea swala la klabu ya Etoile du Sahel katika suala la malipo ya fedha zake, dola 300,000 zaidi ya Sh milioni 630,Fedha hizo ni za malipo ya manunuzi ya mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyeuzwa kwa klabu hiyo ya Tunisia miaka mitatu iliyopita,pia simba imezungumzia swala la mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mbwana Samatta ambaye anakaribia kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji .Kama TP Mazembe watafanikiwa kumuuza Samatta kwa zaidi Tsh Bilioni 6 kwenda KRC Genk, klabu ya Simba itafanikiwa kuvuna Tsh bilioni 1.2 kama ada sehemu ya makubaliano yaliyomo katika mkataba wa mauzo ya Mbwana Samatta aliyeuzwa mwaka 2011 kwenda TP Mazembe akitokea Simba. Mkataba wa mauzo ya Samatta ulikuwa na makubaliano kama TP Mazembe watamuuza Samatta nje ya klabu yao, basi Simba itapata asilimia 20 ya ada ya uhamisho.
MSIKILIZE HAJI MANARA AKIANZA NA SWALA LA SARE
Simba pia wamezungumza juu ya Taarifa zinazosemekana kuwa Klabu hiyo inataka kumsajili mchezaji aliyeachwa na klabu ya Yanga Haruna Niyonzima,lakini Pia Haji Manara ameongelea swala la klabu hiyo kupata matokeo ya Sare katika michezo yao kadhaa ya Ligi kuu.Pia Simba wamezungumzia swala la klabu hiyo kumilikiwa na mtu Binafsi,pia wameongelea swala la ujenzi wa uwanja wa Bunju.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments