Ticker

6/recent/ticker-posts

SOMA ALICHOKISEMA KOCHA WA MANCHESTER UNITED LOUIS VAN GAAL JUU YA KUJIUZULU

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Des.29,2015 SAA 11:34 JIONI
Van Gaal (L) takes his seat next to assistant manager Ryan Giggs (R) at Old Trafford
Meneja wa Manchester United Louis van Gaal, amesema haoni haja ya kujiuzulu baada ya timu yake kutoka sare ya 0-
0 na Chelsea uwanjani Old Trafford.

Van Gaal amekua kwenye shinikizo kubwa La kumtaka kujiuzulu kufuatia kikosi hicho kuchapwa michezo minne mfululizo kipigo cha mwisho kikiwa kutoka kwa Stoke City Jumamosi walipocharazwa 2-0.
Man United wameshindwa kupata ushindi katika michezo minane ya mashindano yote waliyoshiriki msimu huu. Hii ni mara ya kwanza klabu hiyo kufanya hivyo tangu mwaka 1990.
Klabu hiyo kwa sasa imo nambari sita kwenye jedwali na alama tano nyuma ya klabu iliyo nambari nne ligini.
Akizungumza baada ya mchezo kumalizika Van Gaal alisema "Baada ya matokeo haya mashabiki walikuwa wanapongeza. Siwezi kusema kwamba mimi nina wasiwasi sana, lakini katika dunia hii ya soka huwezi kujua.


"kama wachezaji wanaweza kucheza kwa kiwango kile kikubwa,wakiwa kwenye shinikizo hakuna sababu ya kujizulu".
"Mimi niko chini ya mkataba hivyo si suala la kukaa, ni suala la kutimiza mkataba wangu."
katika hatua nyingine  Van Gaal  amesema "Siwezi kuwa na ushawishi wowote juu ya hilo," alisema." nafanya kazi tu na wachezaji wangu na umeona wachezaji wanavyopambana kwa ajili yangu, wao wanafanya vizuri.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments