Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:SOMA ALICHOKISEMA NICOLAS OTAMENDI BAADA YA KUSAINI MIAKA MITANO NA MAN CITY

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.20,2015 SAA 11:10 JIONI

Manchester City wametangaza kusaini mlinzi Nicolas Otamendi kutoka Valencia kwa mkataba wa miaka mitano.



Beki huyo anakuwa usajili wa tatu mkubwa wa City katika kipindi hiki, kufuatia Raheem Sterling na Fabian Delph.Vyanzo vya kuaminika vinasema amesajiliwa kwa ada  £ 33m.

Otamendi, ambaye aliisaidia Argentina kufikia fainali ya Copa America  pamoja wachezaji wenzake Sergio Aguero, Martin Demichelis na Pablo Zabaleta, na amekabidhiwa jezi No. 30.
Manchester City's Txiki Begiristain poses with Otamendi in the board room as he signs his five-year contract


Otamendi aliiambia tovuti ya klabu hiyo:"Nina furaha sana kwa sababu nimekuja katika klabu yenye mvuto wa ajabu. Nafasi ya kucheza katika Ligi Kuu na kufurahia kila mchezo, kusaini katika klabu hii  inaonekana kama maajabu ukiwa nje, kwa sasa nina nafasi ya kufurahia kutoka ndani... ni furaha kubwa kwangu".


"Ilikuwa ni ndoto yangu kupambana katika Ligi ya Mabingwa na kushinda Ligi Kuu."

Meneja Manuel Pellegrini Aliongeza: "Nicolas Otamendi alikuwa ni beki bora katika La Liga msimu uliopita na hivyo kwa kawaida Nina furaha kwa kuongeza mchezaji mwenye ubora kama wake".

 KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments