Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:IVO MAPUNDA AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA,MARA BAADA YA SIMBA SC KUSITISHA MKATABA NA KIPA HUYO,msikilize...

  Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.AUG.17,2015 SAA 01:28 USIKU
Timu ya Simba Sc ya jijini Dar es salaam imesitisha rasmi mkataba na Goli kipa wake Ivo Mapunda mara baada ya pande zote
mbili kukutana,huku uongozi wa Simba ukisema kuwa kipa huyo hakuonesha ushirikiano wakati wanamuitaji kwa mazungumzo ya mkataba mpya.

Ivo mapunda ambaye amejizolea sifa kwa mashabiki wa Timu ya Simba kutokana na uwezo wake Golini, pamoja na mbwembwe zake za kuingia uwanjani na Taulo,amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kumuunga mkono na kuwataka kuelewa kuwa si yeye Ivo Mapunda aliyekataa kusaini Mkataba ,bali viongozi wa Simba Ndio waliyositisha mkataba huo.

"Nidhahili kabisa kwamba huenda walikuwa hawaitaji kupata huduma yangu Tena,kwa sababu nadhani kwa jinsi maelezo nilivyotoa,na wao pia maelezo waliyotoa,ni kwamba kulikuwa na aidha kutokuelewana kidogo ni wapi tukutane au ni muda gani wa mimi kwenda kusaini,si dhani kama kutokuonesha ushirikiana iwe ndiyo sababu ya kutokunipa Fomu niweze kusaini" amesema Ivo Mapunda

MSIKILIZE IVO MAPUNDA AKIONGEA 

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) 

Post a Comment

0 Comments