Mshambuliaji wa timu ya Yanga Amissi Tambwe amehuzunishwa na kitendo cha kunyanyaswa alichofanyiwa na Beki wa Ruvu
Shooting George Michael katika mchezo wa ligu kuu Tanzania akikifananisha kitendo hiko kama ni "Vita" katika Soka.
Shooting George Michael katika mchezo wa ligu kuu Tanzania akikifananisha kitendo hiko kama ni "Vita" katika Soka.
Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo Makao makuu ya Klabu ya Yanga Tambe amesema kama Tanzania kungekuwa na Technologia ya kunasa matukio yanayoendelea katika mchezo,basi wangeona matukio mengi "mabaya"aliyofanyiwa katika mchezo huo.
Tambwe akisema "ni kama unakamata Bastora na kumuoneshea mtu kwenye kichwa,maana yake unamuonesha kama tayari ushamuua" |
Tambwe akionesha Jinsi alivyokabwa |
"Huu sio mpira kwanza,hii ni vita",alisema Tambwe "ni kama unakamata Bastora na kumuoneshea mtu kwenye kichwa,maana yake unamuonesha kama tayari ushamuua" alifafanua Tambwe
Mkuu wa kitengo cha Habari wa Yanga Jerry Muro Akionesha Gazeti linaonesha tukio la kukabwa kwa mchezaji wao Amissi Tambwe |
Tambwe amelalamika kukabwa pamoja na kutolewa maneno ya kibaguzi na Beki wa Ruvushooting George Michael katika mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana,akisema beki huyo alimwambia kuwa yeye ni mkimbizi,jambo ambalo sio kweli kwani yeye anavibali vyote vya kukaa nchini Tanzani.
Kutoka Kushoto:Mwanasheria ni Mwanasheria wa Yanga Frank Chacha,Mkuu wa kitengo cha Habari wa Yanga Jerry Muro pamoja na Mshambuliaji wa wa Yanga Amissi Tambwe |
Uongozi wa klabu ya Yanga umelitaka shirikisho la soka nchini Tanzania Kuwachukulia sheria kali wale wote waliohusika na vurugu katika mchezo huo uliochezwa tarehe 17.jan.2015 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,nakutaka pia Tff kutowapanga tena kuchezesha mechi yeyote waamuzi waliochezezesha mechi hiyo.laa sivyo watagoma kucheza michezo ya Ligi kuu Tanzania.
MSIKILIZE AMISSI TAMBWE AKIZUNGUMZA
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments