Ligi kuu nchini England imeendelea hii leo kwa michezo kadha wa kadha kupigwa katika madimba tofauti tofauti,ambapo mchezo wa
mapema kabisa hii leo ulikuwa ni Arsenal ambapo bao moja la Danny Welbeck Dk.60 limeipa ushindi timu hiyo dhidi ya West Bromwich Albion.
mapema kabisa hii leo ulikuwa ni Arsenal ambapo bao moja la Danny Welbeck Dk.60 limeipa ushindi timu hiyo dhidi ya West Bromwich Albion.
Mchezo wa Manchester United na Hull City umemalizika kwa Man U kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 3 bila majibu katika mchezo uliopigwa katika dimba la Old Trafford.Na mabao ya mashetani hao wekundu yamewekwa nyavuni kupitia kwa wachezaji wake Chris Smalling Dk.16 Wayne Rooney Dk.42 pamoja na Robin van Persie Dk.66.
Chris Smalling of Manchester United
scores the opening goal against Hull despite the best attempts of Allan
McGregor in the Tigers goal
Angel di Maria of Manchester United picks up a hamstring injury against Hull
Mchezaji wa Manchester United Angel Di Maria alitolewa mapema tu mnamo dakika ya 14 baada ya kubanwa na misuli, na nafasi yake kuchukuliwa na Ander Herrera.
Philippe Coutinho of Liverpool runs attempts to beat the Stoke defence at Anfield
Glen Johnson amefanikiwa kuipa ushindi timu yake ya Liverpool kwa bao lake moja alilofunga katika dakika ya 85 katika mchezo huo wa ligi waliokuwa wakicheza na Stoke City katika dimba la Anfield
Nahodha Steven Gerrard alikuwa benchi na kuingia dakika ya 75 kuchukuwa nafasi ya Lucas Leiva.
Mile Jedinak of Crystal Palace (second right) celebrates with team mates as he scores their equalising goal from a penalty
Swansea City wametoka sare ya 1 - 1 na Crystal Palace, walioanza kushinda ni Swansea kupitia kwa Wilfried Bony dakika ya 15 na kisha Mile Jedinak akaisawazishia Crystal Palace kwa penalti dakika ya 25.
West Ham United wakaibuka na ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya Newcastle United,huku Newcastle United wakimaliza pundufu baada ya Moussa Sissoko kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano dakika ya 76,baada ya kufanya madhambi.
Michezo mingine Burnley wakatoka sare ya 1-1 na Aston Villa,na Queens Park Rangers wakaitandika Leicester City mabao 3 kwa 2.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
|
0 Comments