Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.Jun. 11,2014 SAA 11:49 JIONI
Kocha raia wa Italia Roberto Mancini ataondoka kwa magwiji wa Uturuki Galatasaray kwa makubaliano ya pande zote
baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja, klabu hiyo imetangaza siku ya leo Jumatano.
Mancini alijiunga na timu hiyo ya mjini Istanbul kwa mkataba wa miaka mitatu mwaka jana mwezi Septemba, baada ya kufukuzwa na Manchester City mwishoni mwa 2012-13 na kuondoka City baada ya mshtuko kwa kutfungwa katika fainali ya Kombe la FA na Wigan Athletic.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 alichaguliwa na uongozi wa Galatasaray kufuatia kutimuliwa kwa Fatih Terim,na kuchukua usukani siku mbili tu kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa na Juventus.
Hivi karibuni Mancini alisema alitaka kubakia katika klabu hiyo ya Uturuki,na anaondoka baada ya kile kinachoonekana kuwa ni tofauti juu ya maoni yake na mwelekeo wa timu.
"Kama kocha mimi naelewa mahitaji ya klabu Hata hivyo, wakati tunakubalika namna ya kufundisha Gala's walikuwa tofauti," Mancini aliliambia moja ya Gazeti lijulikanalo kama Gazzetta dello Sport
0 Comments