Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.Jun. 11,2014 SAA 07:59 MCHANA
Baraza la wazee wa klabu ya yanga wamewataka wanachama wa klabu hiyo kutowasikiliza baadhi ya watu ambao wanapinga kitendo
cha kumuongezea muda wa mwaka mmoja wa kukaa madarakani Mwenyekiti klabu hiyo Yusuph Manji.
cha kumuongezea muda wa mwaka mmoja wa kukaa madarakani Mwenyekiti klabu hiyo Yusuph Manji.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Mwenyekiti wa balaza la wazee wa klabu ya yanga Mzee Ibrahimu Akilimali amesema kuwa, wanachama ndio waliokubaliana kumuongezea muda mwenyekiti wao Manji,kwani awali mwenyekiti huyo hakutaka kuongeza muda wa kukaa madarakani.
"Tulikubaliana kumuongezea muda wa mwaka mmoja kwa sababu yeye amesema hatagombea.Ndio maana likatokea ombi la wanachama na yeye kulipokea na kukubaliana kumuongezea muda wa mwaka mmoja ili kuweza kumaliza majukumu yake kadhaa" alisema Ibrahimu Akilimali
Adha mzee akilimali akijibu swali la mmoja wa waandishi wa habari la kwa nini wasiitishe mkutano mkuu wa uchaguzi ili kuweza kumpa muda zaidi wa kukaa madarakani, mzee Ibrahimu Akilimali alisema Manji yeye hataki kugombea ndio maana wakampa muda wa mwaka mmoja.
Pia akilimali alipoulizwa kama hawaoni wameisigina katiba kwa kumuongeza muda, alisema kuwa siku zote Hudhuru huvunja sheria.
Mzee Ibrahimu Akilimali amesema hao watu 250 walioandika barua kwa TFF ya kutaka kuitisha mkutano mkuu wa uchaguzi ni wazandiki kwani baadhi yao si wanachama halali wa klabu hiyo, kwani hulalika lakini uwanachama wao wa klabu hiyo umekufa, na kuwataka wawasilishe hiyo barua yao katika Makao makuu ya Klabu ya Yanga,vinginevyo kamati ya maadili itawajadili na kuwafuta uanachama.
0 Comments