NA MWANDISHI WETU, TANGA. IMEWEKWA.Sept.07,2014 SAA 02:00 USIKU
MKUU wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego leo ameongeza
mapokezi ya timu ya Coastal Union yaliyofanyika kwenye
uwanja wa Ndege jijini
Tanga ambapo timu hiyo ilikuwa ikitokea Visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi
kwa muda wa mwezi mzima.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo DC Dendego amesema
kuwa serikali ya wilaya hiyo haitasita kuchukulia hatua watu wote wanaoleta
migogoro na chokochoko ndani ya klabu ya Coastal Union kwa sababu
wasiposhughulikiwa wanaweza kupelekea kuwagawa wanachama,wapenzi na mashabiki hivyo
kudhoofisha maendeleo.
Wachezaji hao walitua uwanja wa ndege Tanga
wakitumia ndege mbili tofauti ambapo baada ya hapo Mkuu huyo wa wilaya aliweza
kuongoza msafara wa magari zaidi ya 50,pikipiki na baiskeli zisizokuwa na idadi
zilizunguka maeneo mbalimbali jijini Tanga huku wananchi wakijitokeza kwa wingi
kuilaki kila ilipokuwa ikipita kwa kuimba nyimbo za kuisifu timu hiyo.
|
ASKARI AKIONGOZA MSFARA WA COASTAL UNION LEO |
|
BURUDANI |
|
KOCHA CHIPO AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI LEO |
|
MAPOKEZI |
|
MSAFARA UKIELEKEA KLABU YA COASTAL UNION |
|
MSAFARA WA PIKPIKI |
|
WACHEZAJI WAKIINGIA KAMBINI |
|
WAPENZI WAKIIMBA AIRPOTI |
Baada ya mzunguko huo ambao ulichukua takribani saa moja ndipo wachezaji wa timu hiyo wakawasili kambini eneo la Raskazone Hotel Pembezoni mwa bahari ya hindi ilipo kambi yao hivyo.
Dendego amesema kuwa lazima wao kama serikali wahakikisha klabu zao mkoani hapa zinakuwa na utulivu kila wakati kwa hiyo inapotokea inakwenda kunyume chake basi wao watachukua hatua kali ili iweza kuwa fundisho kwa watu wengine ambao wanaweza kufanya hivyo kipindi kingine.
|
Kulia ni Kocha Mkuu wa Coastal
Union,Yusuph Chippo akisalimia na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego mara
baada ya kuwasili uwanja wa Ndege Tanga akiwa ameambana na timu hiyo wakitokea
Pemba walipokuwa wamweka kambi wa kwanza kulia anayemtabulisha ni Meneja wa
Coastal Union Akida Machai na kushoto ni Katibu Mkuu wa Coastal Union Kassim El
Siagi |
|
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego
akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege jijini Tanga mara
baada ya timu ya Coastal Union kuwasili katika uwanja huo ikitokea visiwani
Pemba ilipokuwa imeweka kambi ya mwezi mmoja ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi
kuu soka Tanzania bara |
Hata hivyo
amesema kuwa lazima wapenzi ,wanachama na mashabiki kuhakikisha wanakuwa na
mshikamano wa thati ili kuweza kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake
waliojiwekea kwenye msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim
El Siagi amesema kuwa timu hiyo ilifanya usajili mzuri msimu huu hivyo wana
matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwa kuanzia na mechi yao na Simba ambao
haiwapi wasiwasi wa aina yoyote ile.
El Siagi amesema kutokana na maandalizi timu hiyo
walioifanya wakiwa visiwani Pemba wana matumaini makubwa ya kuibuka na pointi
tatu muhimu mbele ya Simba mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu itakayochezwa uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
|
ALIYEKUWA MWENYEKITI WA COASTAL UNION HEMED AURORA KULIA AKITETA JAMBO NA
MKUU WA WILAYA YA TANGA HALIMA DENDEGO LEO KWENYE MAPOKEZI HAYO |
Awali akizungumza katika mapokezi hayo,aliyekuwa
Mwenyekiti wa Coastal Union,Hemed Aurora amewataka wapenzi ,wanachama kudumisha
na kuendeleza mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuweza kufikia malengo yao ya
kuchukua ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Umoja na
mshikamano ndio siri ya mafanikio yoyote yale hivyo nawasihi wapenzi ,mashabiki
na wanachama muenzi mshikamno kwa sababu ndio nuru ya mafanikio kwenu “Alisema
Aurora.
KWA TAARIFA,MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,BREAKING NEWS,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
PICHA ZOTE NI KWA HISANI YA COASTAL UNION
0 Comments