Kamati ya Rufani ya shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF
limemrudisha katika kinyang'anyiro cha uchaguzi Michael Richari Wambura ambaye alienguliwa na kamati ya uchaguzi ya Simba kwa sababu za kutokuwa mwanachama wa klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mchache uliopita Mwenyekiti ya rufani ya TFF Julius Lugaziya amesema Kuwa Wambura ni mwanachama halali wa klabu Simba, kwani amekuwa akishiriki katika mikutano yote ya simba kama mwanachama,isipokuwa mkutano wa uchaguzi,na pia amekuwa akilipa ada zote za uanachama.
Aidha Lugaziya amehoji kuwa,kama Wambura si mwanachama wa Simba,iweje awepo katika kamati ya utendaji ya Simba ambayo ndiyo iliyoichagua kamati hiyo ya uchaguzi?

"Maamuzi huamuliwa kwa kura kama wajumbe hawakufikia maamuzi na ndio kilichofanyika" alisema Julius Lugaziya
Pia kamati ya rufani ya Tff imetoa wito kwa kamati za uchaguzi za klabu kufuata kanuni na kuacha kujali maslai ya watu binafsi, na kusema kamati ya uchaguzi ya simba ilikuwa batili kwani haikufuata kanuni kwa kumsimamisha Wambura.

Mwisho wa yote kamati ya rufaa ya Tff chini ya mwenyekiti wake Julius Lugaziya imesema,inabadilisha maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba kwa kumrudisha wambura katika kinyang'anyiro cha uchaguzi.
0 Comments