Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez hajui ni wakani gani
mshambuliaji Luis Suarez, atakuwa vizuri na kuwa tayari kurudi kufanya kazi baada ya goti lake kufanyiwa upasuaji, aliyasema siku ya jana Jumanne.
Tabarez alisema " Amerudi vizuri sana na anaweza kuwa bora,anafanya kazi ya ziada nje mazoezi yake kimwili.,"
"hatuwezi kutajaa tarehe kamili, mimi sijui kama tutaweza kuwa naye kwa ajili ya mechi ya kwanza, ya pili, na ya tatu,Kama ingekuwa ni juu yangu, Suarez angecheza kesho." Tabarez aliwaambia waandishi wa habari baada ya mazoezi ya Uruguay
Uruguay katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia katika kundi D watakipiga dhidi ya Costa Rica na kufuatiwa na mechi dhidi ya England na Italia.
Suarez aliwaambia mashabiki wake katika Twitter kuwa amewasili katika kikosi nchini Brazil na anajisikia nafuu katika goti lake la kushoto yuko tayari kurudi kwa ajili ya kombe la dunia
Suarez aliwaambia mashabiki wake katika Twitter kuwa amewasili katika kikosi nchini Brazil na anajisikia nafuu katika goti lake la kushoto yuko tayari kurudi kwa ajili ya kombe la dunia
0 Comments