Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 04,2014 SAA 11:12 ALFAJIRI
Christian Benteke atafanyiwa upasuaji wa majeraha ya kisigino yatakayompelekea kukaa nje hadi mwisho wa
msamu na kumfanya pia kukosa msimu wa fainali za kombe la Dunia,klabu ya Aston Villa imethibitisha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliumia wakati wa mazoezi siku ya Alhamisi na kuthibitishwa kuwa, ameumia kwa kiwango kikubwa, ambapo klabu ilisema atakuwa nje "kwa kiwango cha kukadilia miezi sita"
"Ni pigo kali kwetu sote kwa Christian na kwa klabu," bosi Paul Lambert aliiambia tovuti rasmi ya klabu hiyo.
"Atakosa mapumziko ya msimu, ni wazi, na pia Kombe la Dunia. Lakini itambidi kufanya kazi kwa bidii kwa sababu hiyo ndiyo atafanya kurudi kwetu na nguvu zaidi ya hapo msimu ujao."
Benteke alikuwa na wakiti mzuri katika msimu wake wa kwanza akiwa England, kwa kufunga mabao 28 katika mechi 50 akiwa na Villa na Mbelgiji huyo ameisaidia klabu yake kuhifadhi hali yao ya Ligi Kuu na nchi yake kufika Brazil.
0 Comments