Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:FAHAMU MKATABA MPYA WA KOCHA WA STARS,ALICHOKISEMA NDOLANGA,MALINZI NA KOCHA MWENYEWE

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 26,2014 SAA 04:57 USIKU
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij Mart Nooij kutoka
Uholanzi,ametambulishwa hii leo (Aprili 26 mwaka huu) na Rais wa shirikisho la mpira Tanzania Jamal Malinzi kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akimtambulisha mbele ya waandishi wa habari hii leo Jamal Malinzi amesema wameamua kumchukuwa kocha huyo kutoka uholanzi kwani ana mafanikio makubwa katika bara la Afrika,na pia historia ya Uholanzi katika ulimwengu wa soka haina mfano.


Aidha Malinzi ameoongeza kuwa,anawaahidi wa Tanzania kuwa hawataingilia majukumu ya kocha huyo,kwani kufanya hivyo ni kuvuruga utaratibu wa kocha huyo.


"Nimemwambia mwalimu kama kuna mtu atamuingilia kazi yake,aniambie"
Muhidin Ndolanga(kushoto) na Wallace Karia(kulia)
Naye kiongozi wa zamani katika soka Mzee Muhidin Ndolanga amemuunga mkono Jamal Malinzi kutomuingilia kocha huyo katika kazi yake,kwani kufanya hivyo ni kusababisha matatizo katika mchezo.
Kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Martinus Ignatius Maria maarufu kama Mart Nooij 
Naye kocha huyo mpya wa Tanzania Mart Nooij amesema ameamua kuja kufundisha mpira Tanzania akiamini anakuja kuleta mafanikio makubwa,kwani mpira ni kokote pale na amefanya kazi katika nchi nyingi za kiafrika.
Viongozi mbalimbali wa mchezo wa soka Tanzania walikuwepo
"Kwangu mimi ni fahari kuwa hapa,na nina matumaini na shirikisho pamoja na serekali kwa ujumla na pia natumaini nitaleta mafanikio katika soka" alisema Mart Nooij.

Nooij ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili  ameongeza kwa kusema kuwa yeye ni mtu wa maneno mafupi, hawezi kuahidi kitu lakini ana matarajio ya kuifanya Taifa Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.

Amesema kabla ya kukubalia kufundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia, lakini vilevile amewahi kufundisha mpira wa miguu barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Mali na Msumbiji.

Post a Comment

0 Comments