Manuel Pellegrini alifanya moja ya jaribio la mwisho kwa kuiweka njia panda kwa pressure timu
ya Liverpool kwa kudai kuwa Liverpool wamepoteza uongozi wa ligi kuu.
ya Liverpool kwa kudai kuwa Liverpool wamepoteza uongozi wa ligi kuu.
Meneja huyo wa Manchester City pia alisisitiza wachezaji wake - ikiwa ni pamoja na Samir Nasri, ambaye alipatiwa tiba kidogo ya kawaida katika uwanja wa mazoezi wa Carrington -kuwa wanaamini bado wanaweza kubadili matokeo na kuitoa Liverpool katika uongozi wa ligi kuu.
Nini kinaendelea hapa? Samir Nasri anapata matibabu katika uwanja wa Carrington huku Manuel Pellegrini akimuangalia |
Pressure:Pellegrini anasema City wako tayari kunyakuwa uongozi kutoka kwa Liverpool |
City imeonekana kukosa nafasi baada ya kupoteza katika uwanja wa Anfield na kufuatia kuwa na matokeo ya mshtuko kwa kutoka sare ya nyumbani dhidi ya Sunderland, lakini Pellegrini anasisitiza bado yuko katika mawindo.
Joe Hart akipiga tizi |
Viongozi: Pellegrini akitabasamu na nahodha wake Vincent Kompany katika mazoezi kabla ya kukutana na Crystal Palace |
Akijiandaa kwa ajili ya safari ya kupambana na Crystal Palace, Pellegrini alisema: "Kama Liverpool wakishinda michezo yao mitatu iliyobaki, wao ni mabingwa, hivyo watakuwa na faida. sisi tulipoteza katika uwanja wa Anfield, imetuweka katika nafasi kwa mara ya kwanza ya wasiwasi".
"Lakini wachezaji wetu bado wana imani kwamba wanaweza kushinda Ligi. Wote wana amini. Kila mtu anayefanya kazi katika mchezo anajua kwamba katika mpira wa miguu, kitu chochote kinaweza kutokea, hasa katika michezo mitatu iliyobaki, ambapo pressure ipo".alisema anuel Pellegrini.
0 Comments