Ticker

6/recent/ticker-posts

LIGI YA MABINGWA:GUARDIOLA AMESEMA MANENO HAYA KWA REFA BAADA YA BASTIAN SCHWEINSTEIGER KUONYESHWA KADI NYEKUNDU

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 02,2014 SAA 03:28 ASUBUHI
Kocha wa Bayern Munich  Pep Guardiola amehudhunishwa na refa kwa kumuondoa  Bastian Schweinsteiger katika sare
ya bao 1-1 dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford  akisema kwamba 'hakufanya haki'.

United  walionyesha ushujaa katika mechi yao kwanza ya ligi ya mabingwa barani ulaya katika robo fainali, na watakwenda  Allianz Arena wiki ijayo kwa matumaini ya kufikia hatua ya nusu fainali.

Nemanja Vidic alikifanya kikosi cha David Moyes kuongoza kwa bao lake D.k58, lakini Schweinsteiger akasawazisha Dk 67, kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya mwisho, kwa maana yake atakosa mchezo wa marudiano.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Germany alipewa na kadi ya njano kwa mara ya pili baada ya changamoto na Wayne Rooney, na alionyesha kuchanganyikiwa  wakati huo na kuonekana kuonyesha kuwa alimuona mshambuliaji huyo wa England kuwa alijiangusha.

Guardiola hakutaka mjadala kuhusu tukio hilo lakini alimsema Kihispania mwamuzi Carlos Velasco Carballo kuhusu jambo hilo.

Bosi huyo wa zamani wa Barcelona alisema: "Mimi nilizungumza na mwamuzi na yeye alinipa maoni yake ... na  heshimu (hilo)."

Alipoulizwa kama yeye alikubaliana na uamuzi, alisema: "Bila shaka hapana."

Alipoulizwa kuhusu Schweinsteiger  dhahiri alionyesha ishara ya kujiangusha 'kupiga mbizi', alisema: "Mimi sikuweza kuiona, lakini nilizungumza na mwamuzi".

"Yeye ni mwamuzi mzuri sana. alichezesha mchezo vizuri sana, lakini hakufanya haki".


"Lakini ni sawa. Ili kushinda Ligi ya Mabingwa unatakiwa kukabiliana na kila kitu. Katika soka ya aina hii ni kitu kinachotokea."

Kwa ujumla, Guardiola alifurahishwa na kazi ya vijana wake,na kuamini wana nafasi ya kufanya vizuri katika mpambano wa pili.

Akasema: "Matokeo yake ni 1-1 hivyo sisi tumeshinda ugenini, hivyo hii ni nzuri Nina furaha kwa ajili ya utendaji wetu, asilimia 70 tumemiliki, 15 tumejaribu"..

" si rahisi kutengeneza nafasi lakini sisi tulitengeneza za kutosha kabisa".
"Tulikuwa Tukijibu baada ya kufungwa 1-0.  sio matokeo ya kepekee lakini ni mazuri vya kutosha ukizingatia jinsi ya uzuri wa Manchester United ."


Post a Comment

0 Comments