Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 02,2014 SAA 11:55 JIONI
Uongozi soka ulimwenguni umechukua hatua dhidi ya mabingwa wa Primera Division pamoja na FA ya
Uhispania kwa ukiukaji unaohusiana na uhamisho wa kimataifa wa wachezaji wanachipukia.

Barcelona wamepigwa marufuku na FIFA kusaini wachezaji katika vipindi viwili vya uhamisho yaani miezi 14(majira 2014 na Januari 2015) kwa ukiukaji huo unaohusiana na uhamisho wa kimataifa na usajili wa wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18.
Vikwazo hivyo vinafutiaa uchunguzi wa awali uliofanywa na kitengo cha uhamisho cha Fifa (Fifa TMS) katika kipindi cha mwaka jana na hatimaye kamati ya nidhamu ya Fifa kufanya uamuzi huo kama sehemu ya kesi za kinidhamu.
Barcelona wamepatikana na hatia ya kukiuka masharti kadhaa kuhusu uhamisho wa kimataifa na usajili wa mwanzo wa watoto wa Kihispania wa klabu hiyo, pamoja na kanuni nyingine muhimu kuhusiana na usajili na ushiriki wa wachezaji fulani katika mashindano ya kitaifa.
Kamati ya Nidhamu imeweka vikwazo vya uhamisho katika klabu hiyo na kupigwa marufuku katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa vipindi viwili mfululizo vya uhamisho, pamoja na faini ya CHF 450,000 (369,000 €).
Zaidi ya hayo, klabu imepewa muda wa siku 90 za kuhalalisha hali ya wachezaji wote madogo husika katika klabu hiyo.

0 Comments