Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA.APR. 18,2014 SAA 02:37 USIKU
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney
ametangazwa kuwa fit kwa ajili ya kwenda kukipiga dhidi ya klabu yake ya zamani Everton siku ya Jumapili.
Mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kidole cha mguu wake wa kushoto toka katika mchezo wa kwanza waliotoka sare 1-1 dhidi ya Bayern Munich tarehe 1 Aprili katika Ligi ya Mabingwa UEFA.
Mshambuliaji Robin van Persie bado atakuwa kando baada ya kuumia goti, ni nafasi kubwa kwa meneja David Moyes kuhakikisha timu yake inapambana ili kufuzu klabu bingwa Ulaya msimu ujao na michezo minne iliyobaki.
Moyes alisema: "Wayne Rooney ilikuwa katika mazoezi makubwa wiki hii, Yuko katika fomu mzuri Kurudi ni jambo jema".
"alikuwa hayuko vizuri na kidole chake wakati wa mchezo wa mwisho."
Alipoulizwa kama Rooney atakuwa katika kikosi cha kusafiri kwenda Goodison Park, Moyes alijibu: "Ndiyo."
Moyes hakuwa katika hali nzuri wakati wa mechi yake ya kwanza kurudi katika uwanja wa Goodison Park tangu kuondoka katika klabu hiyo mwisho majira ya joto na pia alitoa habari kwamba Van Persie amepata mandeleo mazuri katika matibabu yake baada ya kuumia goti katika mechi dhidi ya Olympiakos,sasa anatarajiwa kurudu labda wiki ijayo na si tena wiki nane au sita za kukaa nje
Moyes alithibitisha kuwa kiungo Marouane Fellaini amepona baada ya kuumia ndama na pia atakuwa fit kuikabili klabu yake ya zamani.
Moyes pia alisema Rafael atakuwa nje kutokana na tatizo la mguu wakati Jonny Evans kunamashaka makubwa kuwepo katika mechi hii ,kwa sababu ana sumbuliwa na tatizo la muda mrefu la kuumia ndama .
0 Comments