Ticker

6/recent/ticker-posts

YALIYOWATOKEA YANGA,SASA YANAWAKUTA TIMU YA NKAMA KUTOKA ZAMBIA

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 27,2014 SAA 01:18 JIONI
Moaamen Zakrya Abbas
Timu kutoka  Zambia Nkana itakutana na arch-Nemesis Zamalek ya Misri katika hatua ya kufa au kupona  katika michuano ya Ligi
ya Mabingwa barani Afrika hatua ya nyingue,baada ya kuamuliwa mchezo wao kupigwa katika mji wa Alexandria siku ya Jumapili.

Timu zote mbili zitapambana milango ikiwa imefungwa na bila mashabiki, katika uwanja wa Haras El Hodod,  ambapo mechi hiyo imebadilishwa kutoka uwanja wake wa awali katika uwanja wa kimataifa ilioko mjini Cairo kwa sababu za kiusalama katika mji mkuu wa Misri.

Zamalek na Nkana wataerekea Alexandria wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya 0-0 kutoka katika mchezo wa kwanza uliocheza Machi 22  katika uwanja wa Nkana ulioko mjini Kitwe.

Post a Comment

0 Comments