Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger anasema kwamba utendaji wao wa kazi wa kesho dhidi ya Manchester City
utaonyesha kwamba wao hawajakata tamaa ya kushinda Ligi Kuu.
Arsenal wanakwenda katika mchezo dhidi ya City,wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo kwa mabao 6 kwa 0 dhidi ya Chelsea nakutoka sare ya 2 - 2 na timu ya Swansea.
Wenger aliweka wazi mipango yake ya muda mrefu na alisema kuwa yeye analenga kuziba alama sita zilimweka pengo - na viongozi wa ligi Chelsea - katika michezo saba iliyobaki .
"Hakuna kipaumbele kingine zaidi ya kushinda kwanza," alisema Wenger. "Hilo bado ndio lengo letu".
"Mabingwa huendelea ikiwa mtu mwingine anawakatisha tamaa. Tuna nafasi ya kuonyesha kwamba tuna uwezo wa kiakili".
"Kama watu wanasema Everton wanaweza kutupata basi sisi tunaweza kuipata timu ya juu yetu. Sisi hatuja kata tamaa, amini kwangu. Ni mtazamo wetu kesho ambao utaonyesha".
"Ni mchezo mwingine ambao kweli ni muhimu sana, na mchezo mwingine ambao pia una umuhimu mkubwa kwa sababu Man City na wao wanapambana katika nafasi ya juu".
"Wao ni washindani wanaochukuliwa kuwa na uwezo wa kushinda ligi na Chelsea pamoja na Liverpool, lakini wakati wewe unacheza na mmoja wenye uwezo wa kushinda, una nafasi ya kufupisha umbali kwao."
Arsenal walipigwa 6-3 katika uwanja wa Etihad mwezi Desemba lakini hawajapoteza mchezo wa ligi wakiwa nyumbani tangu siku ya ufunguzi wa msimu, na Wenger alisema: "Sisi tutacheza katika uwanja wa Emirates ambapo sisi tutaonyesha uwezo mkubwa na tunataka kuonyesha mchezo". .
0 Comments