Ticker

6/recent/ticker-posts

HIKO NDICHO ALICHOKIFANYA PETER ODEMWINGIE KWA KOCHA WAKE STEPHEN KESHI

Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 26,2014 SAA 01:10 USIKU
kocha mkuu wa Super Eagles ya Nigeria  , Stephen Keshi amebaini kwamba msambuliaji wa Stoke City, Peter Odemwingie ameomba
radhi kufuatia kuibuka kwa taarifa kuwa alikuwa ametengwa katika kikosi cha Nigeria kwa ajili ya kombe la mataifa ya Afrika 2013.

Mchezaji huyo mwenye miaka 32   alitumia mitandao wa  kijamii wa  Twitter, kumkosoa Keshi baada ya kuweka wazi hawezi kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya  A FCON 2013 na kikosi cha Super Eagles.

Keshi alisema alikuwa akizungumza na mshambuliaji huyo kufuatia tukio hilo na  kusisitiza kwamba "kamwe hakukua na  tatizo lolote kati yetu".

Post a Comment

0 Comments