Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 26,2014 SAA 12:25 JIONI
Rais wa Inter Milan Erick Thohir amesema kuwa Bacary Sagna ataendelea kubaki katika ligi kuu ya England msimu
huu.
Thohir aliweka wazi mapema wiki hii kuwa , Inter walikuwa na mazungumzo kuhusu kumsaini beki huyo wa Arsenal , ambaye mkataba wake unafikia mwisho, mwishoni mwa msimu.
Hata hivyo, anaaminika kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 ameamua kubaki katika Ligi Kuu baada ya kukataa majaribio ya Inter kutaka kumshawishi amehamie San Siro.
"Nadhani (Bacary) Sagna hataweza kuwasili kwa sababu yeye ameamua kukaa katika Ligi Kuu England ," Thohir aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Milan.
"Kwa sasa tuko tu na (Yuto) Nagatomo na Jonathan. Kama mmoja wao akipata majeruha,anahitajika mtu mwingine kuja hapa".
"Lakini tuna kukubali ukweli kuwa (Sagna) anataka kukaa nchini Uingereza,tunaelewa katika kesi kama hii, sisi tutamchukuwa mchezaji kijana kutoka katika academy yetu."
Na sasa bado inaonekana kama nafasi ya Sagna kubaki katika klabu hiyo ya Uingereza, kama hana, kana kwamba atakuwa na Arsenal msimu unaofuata, baada ya wapinzani wao wa Ligi Kuu , Chelsea na Manchester City walikuwa wanaohusishwa na kutoa ofa kwa mchezaji huyo.
0 Comments