Mhariri:Herman kihwili,IMEWEKWA March. 26,2014 SAA 05:20 USIKU
Mchezaji wa Zamani wa Manchester United Eric Cantona anaamini kwamba timu hiyo itarudi na kuleta heshima
kubwa hivi karibuni.
kubwa hivi karibuni.
United wana pointi 12 nyuma ya timu ya Arsenal inayoshika nafasi ya nne baada ya kufungwa mabao 3-0 na Manchester City siku ya Jumanne, na timu hiyo iko katika hatihati ya kukosa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Mabingwa wa sasa Bayern Munich watakutana na klabu hiyo ya Old Trafford katika nusu fainali ya Ligi ya mabingwa, lakini mashabiki wa United wameshakata tamaa juu ya matarajio ya kukosa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
![]() |
Eric Cantona |
Cantona alisema: "Manchester United ni moja ya klabu kubwa katika dunia, Wamekuwa katika ngazi ya juu kwa miaka 20, na nadhani wao watarudi tena, hivi karibuni"..
Na Cantona anaamini David Moyes atapewa muda wa kujenga kikosi cha United baada ya msimu wake kwanza kuwa mgumu katika kazi yake, baada ya kuchukuwa nafasi ya Sir Alex Ferguson mwishoni mwa majira ya joto".
Paul Scholes pia anahisi United lazima wakae na David Moyes,na kumasaidia katika harakati za Usajili.
Moyes tayari ametumia £ 27.5million kwa ajili ya usajili wa Marouane Fellaini na £ 37.1million kwa ajili ya usajili wa Juan Mata tangu kuchukua hatamu katika timu hiyo ya Old Trafford.
0 Comments