Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 12.2013 SAA 03:51 USIKU
Zambia
watajaribu kujikomboa wenyewe katika Kombe la CECAFA 2013 nchini Kenya
wakati wao watakapokutana na timu
ya Tanzania katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na wa nne,mchezo utakaochezwa siku ya Alhamisi katika mji wa Nairobi.
Chipolopolo
wameshindwa kuhitimu kwa fainali ya Kombe la CECAFA siku ya Jumanne
baada ya kufungwa mabao 2-1
na Sudan katika mji wa Mombasa.
Zambia watakutana siku ya Alhamisi pia kwa mara ya pili na Tanzania katika
mashindano ya mwaka huu.
Zambia mapema walitoka sare ya 1-1 na Tanzania katika mchezo wa kufungua kwa pande zote mbili wa Kundi B, Novemba 28 mjini Machakos.
Sare
pia iligeuza pointi kwa Zambia,na kocha Patrice Beaumelle ambaye alijiunga hivi karibuni kama kocha mkuu, baada ya kupoteza michezo yake ya awali
mitatu kabla ya kujiingiza katika mechi ya nne na kutamba kuwa hasira zake angezimalizia kwa Sudan.
"Kwanza
tumepata nafuu kutokana na kushindwa, tumesikitishwa lakini
lengo letu ni kupata nafasi ya tatu," Beaumelle alisema.
Wasiwasi mkubwa kwa Zambia ni jinsi ya kuokoa haraka mchezo wao wa
mwisho masaa 48 tu baada ya kutoka-nyuma kwa kushindwa.
0 Comments