Ticker

6/recent/ticker-posts

MOYES ASEMA HANA HOFU NA KIKOSI CHAKE

 Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 21.2013 SAA 05:04 ALFAJIRI
Bosi wa Manchester United  David Moyes anasisitiza kuwa  hakuna hofu katika kikosi chake na wao wanachojalibu ni kuzuia kufungwa
moja kwa moja katika ligi katika uwanja wa Old Trafford.

United waliopotea michezo mitatu mfululizo ya ligi katika uwanja wa  Old Trafford tangu mwaka 1979.

Patrice Evra anasema ana imani kuna kuongezeka kwa hofu  katika michezo ya nyumbani, lakini Moyes hakubaliani na mchezaji  huyo.

"Matokeo hayo,sisi hatuyataki," alisema Moyes. "Kwa sababu hiyo, maneno kama hayo, yanaleta mazingira magumu, wasiwasi wote kuja akili."

"Lakini binafsi sijawahi kupatikana kama hivyo. Mashabiki huwa wanaunga mkono timu. Wanajua tunahitaji kucheza vizuri na sisi tuna haja ya kufunga kwa magoli zaidi, lakini haijawahi kwa kutaka kujaribu." 

United ni dhahiri watakuwa bila Nani, ambaye tayari amejiunga katika orodha ya majeruhi wa muda mrefu, na Moyes amethibitisha kuwa mreno huyo aliyezaliwa Praia, Cape Verde  atakuwa nje "kwa muda wa wiki chache"  kutokana na matatizo ya misuli. 

Kwa upande mwingine, Wayne Rooney "ana nafasi" ya kupona kutokana na matatizo ya paja ambayo yalimuweka nje katika mchezo wa robo fainal ya Capital One Cup dhidi ya Stoke katikati ya wiki hii.
 
Mchezo wa Jumamosi ni mechi ya mwanzo wa mechi nne  ambazo United wanamatumaini ya kuboresha na kupata bahati yao.

Kwa wengine watasema ,soka limewazidi. Hata hivyo Moyes anakumbuka wakati ambapo ilikuwa mbaya zaidi.

 "Nakumbuka siku wakati imenitokea kwa haraka zaidi,nilipoteza michezo miwili katika siku mbili," alisema mscot huyo.

"nilicheza katika hali kama hiyo.tuna lalamika sasa kwa sababu ni siku mbili kwa tatu, lakini tutatumika kucheza wakati wa Krismasi katika nchi yetu." alimalizia kusema David William Moyes.



 

Post a Comment

0 Comments