Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Yusuf Manji amemtetea mlinda mlango wa timu hiyo aliyesajiliwa katika dirisha dogo Juma
Kaseja kwa kusema kuwa hawakumsajili mlinda lango huyo kwa ajili ya kuifunga timu ya Simba.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo iliyoko makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani siku moja baada ya kufungwa 3 -1 na watani wao wa jadi,Manji amesema hawakumsajili Kaseja kimakosa bali ni kwa ajili ya kuweza kuwasaidia katika mechi za kimataifa na si kwa kuifunga Simba,na kuongeza kuwa mechi ya Nani Mtani Jembe iliyofanyika jana ilikuwa ni Bonanza tu.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji.
Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa
matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi
iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa kusema anajua kuwa wanachama, na wapenzi wameumia sana na hakuna aliyefurahishwa na
matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi
unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari hii leo(hawapo pichani) makao makuu ya klabu hiyo, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga |
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa
kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza
wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa
takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao
hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa
hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa
jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokeza katika
mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye
anasafiri leo kwenda nje ya nchi majukumu yote amemkabidhi makamu
mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.
0 Comments