Mhariri:Herman Kihwili.IMEWEKWA DESEMBA 23.2013 SAA 08:40 USIKU
Huu ni wakati wa upendo na mapenzi ya kweli, ndoa ya mume aliyekuwa mgonjwa mahututi hospitalini iliyofanyika katika kitanda
chake.
Cola
Glenny mwenye umri wa miaka 22, alisema 'mimi ni wa Felix Glenny",mwenye umri wa miaka 23, aliyekuwa amelazwa
katika kitanda cha Hospitali ya Medway Maritime, akiwa anasumbuliwa na kansa
ya tumbo iliyoshindikanika.
Sherehe: Felix Glenny akifunga ndoa na Cola Glenny katika sherehe iliyofanyika Medway Maritime Hospital juzi |
Felix
alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo nje ya kitanda chake kusherehekea
'siku yake kamili' baada ya hapo na mke wake mpya, wakati watoto wao wawili
Ralph mwenye miaka miwili na Pearl mwenye miezi minne wakiwepo.
'Ni kamili': wawili wamefinga ndoa katika Hospital Medway Maritime, ambapo Felix imekuwa huko tangu Novemba |
Alilazwa hospitalini Novemba baada ya kuugua ugonjwa kwa muda wa wiki
kadhaa, na mara ya kwanza walidhani amepatwa na ugonjwa tu wa tumbo.
Lakini baada ya kulazwa hospitalini tarehe 11 Novemba, madaktari walimpata na tatizo hilo kubwa katika tumbo lake.
Ingawa alikuwa na uwezo wa kuondoka, vipimo zaidi vilionyesha kuwa kansa ilikuwa imeenea kwa Felix kwa wiki alizoishi.
Baada
ya kupita wiki kansa ilizidi kusambaa, Felix na Cola waliamua kuoana haraka iwezekanavyo, na waaliwaalika marafiki zao pamoja na familia zao na kufunga ndoa iliyofungishwa na mchungaji hospitalini siku ya jumamosi ya tarehe
Kusambaa: Felix alipatikana na kansa,ilikuwa mbaya sana na iku ya Ijumaa iliyopita wazazi hao wa watoto wadogo wawili, walitaka kifunga ndoa haraka iwezekanavyo |
Akizungumza na MailOnline usiku wa jumapili tarehe 22 , Cola alisema: "Baada ya operesheni ya pili ya siku ya Ijumaa ya mwisho, waligundua kwamba kansa ilikuwa emeenea kila mahali. Hivyo sasa,haiwezekani kuutokomeza ugonjwa huo."
"walituambia tunatakiwa kuondoka katika chumba - ilikuwa imemchukuwa sana".
"Baada
ya mipango yote kushindikana,tulizungusha vichwa vyetu pande zote, ni kama vile
tunaweza, Felix alisema alitaka tuoane haraka kama tunaweza.Tukafunga ndoa siku ya jana"
"nilichanganyikiwa kwa sababu tulikuwa na furaha, lakini nilikuwa na hisia za kweli."
"Ilikuwa ni siku nzuri na tumekuwa tukifikiri juu yake leo", alisema
"Ilikuwa imetimia na hakuweza kwenda popote".
"Tulikuwa tukizungumza kuhusu kufunga ndoa hata kabla ya yeye kuwa
mgonjwa - na wakati tulipogundua kansa imeenea tukataka kufanya
hivyo mara moja".
"Felix ameweza kutoka nje ya kitanda na tukaenda ndani ya klabu ya kijamii
na tukawa na sherehe -.viongozi wa dini ambao wanafanya huduma za kidini hospitalini walikuja na walitupa
baraka"
'Ilikuwa ni siku nzuri kweli na kila mtu alitusaidia.Wote wa familia yetu walikuwepo hapa na marafiki zetu wengi."
Inahusu?: Felix alikuwa na uwezo wa kuondoka katika kitanda chake cha hospitali na kukata keki ya harusi na kumpiga busu bibi yake mbele ya marafiki na familia |
Felix, ambaye pia anajulikana kama Ryan, alikutana kwa njia ya rafiki yao waliyeheshimiana mjini Stoke, Kent, mwezi Agosti 2010.kwa
haraka wakapendana na ndani ya mwaka wanandoa hao wakiwa pamoja, Cola alikuwa na mimba ya mtoto wake wa
kwanza, Ralph.
Baba wa kujivunia: Felix kabla ya yeye kulazwa hospitalini, akiwa na mwanawe Ralph, (kushoto), na mtoto wa kike Pearl
|
Cola ambaye mfanyakazi wa saloon za kina mama, na Felix ambaye anafanya kazi katika kampuni ya kusambaza maji,waliishi kwa furaha pamoja kwa miaka miwili na walikuwa na mtoto wa
pili, Pearl, ambaye sasa ana umri wa miezi minne.
Mhariri:Herman Kihwili
0 Comments